Taarifa ya habari 23 Juni 2020

Bango la taarifa ya habari la SBS

Bango la taarifa ya habari la SBS Source: SBS

Wakati maambukizi ya COVID-19 yaongezeka Victoria, wakazi wa Kusini Australia waregezewa vizuizi vya COVID-19.


Rais wa Marekani Donald Trump ameongeza muda wa kusitishwa kwa visa za bahati nasibu pamoja na zile za wafanyikazi wa kigeni hadi mwisho wa 2020.

Raia wa Malawi wanapiga kura leo katika awamu ya pili ya uchaguzi wa urais, miezi mitano baada ya mahakama ya katiba kufuta matokeo ya uchaguzi wa mwaka jana.

Saudi Arabia imepiga maarufuku raia kutoka mataifa mengine kufanya ibada ya Hija nchini humo mwaka huu ili kudhibiti virusi vya corona. Ni idadi ndogo tu ya watu wanaoishi kwa sasa katika ufalme huo watakaoweza kushiriki Hija, kulingana na tangazo lililotolewa kwenye vyombo vya habari vya taifa hilo.


Share