Jimbo la Magharibi Australia lita endelea kufungwa katika msimu wa likizo, wakati mipango yakufunguwa jimbo hilo itazangatiwa tu wakati 90% ya wakaaji watakapo kuwa wamepata chanjo kamili jimbo humo.
Waziri wa Mambo ya Nje wa Marekani Antony Blinken alitangaza leo Ijumaa kuwa Rais wa Marekani Joe Biden anapanga kuanda mkutano na viongozi wa Afrika ili kuonyesha dhamira ya Marekani kwa bara hilo. Hatua hiyo iinatokea wakati China ikiongeza ushirikiano na Afrika ikiwa ni pamoja na kupitia mkutano mkuu mwezi huu nchini Senegal, ambapo Blinken anaongoza baadaye Ijumaa. Washirika wa Marekani Ufaransa, Uingereza na Japan pia wamekuwa wakifanya mikutano ya mara kwa mara na viongozi wa Afrika.
Maafisa wa kijeshi na serikali nchini Sudan wamesema leo kuwa makubaliano yameafikiwa kati ya viongozi wa kijeshi na kiraia kumrejesha madarakani waziri mkuu aliyeondolewa madarakani katika mapinduzi ya Oktoba 25 Abdalla Hamdok. Viongozi hao wameongeza kuwa maafisa wa serikali na wanasiasa waliokamatwa tangu mapinduzi hayo wataachiwa huru kama sehemu ya makubaliano hayo kati ya jeshi na vyama vya kisiasa, ikiwa ni pamoja na Chama kikubwa cha Umma.