Taarifa ya habari 21 Juni 2020

Bango la taarifa ya habari la SBS

Bango la taarifa ya habari la SBS Source: SBS

Jimbo la Victoria larejesha tena vizuizi vya coronavirus, baada ya ongezeko ya maambukizi katika jamii.


Rais Abdel Fattah al-Sisi wa Misri ameonya kwamba nchi yake ina uhalali wa kuingilia nchi jirani ya Libya, na ameliamuru jeshi lake kuwa tayari kwa operesheni ya nje ya nchi, ikiwa italazimika.

Msaidizi mkuu wa Rais Felix Tshisekedi wa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo, amehukumiwa kifungo cha miaka 20 jela na kazi ngumu kutokana na hatia ya ufisadi, katika kesi ya aina yake.

Waziri wa zamani wa mambo ya nje wa Tanzania Bernard Membe, amesema yuko tayari kuingia katika kinyang’anyiro cha ugombea urais kupitia chama tawala cha CCM mwaka huu, endapo kamati kuu ya chama hicho itatoa tamko kwamba hajafutiwa uanachama wake.


Share