Taarifa ya habari 21 Julai 2020

Bango la taarifa ya habari la SBS

Bango la taarifa ya habari la SBS Source: SBS

Mpango wa ruzuku ya mshahara wa serikali ya shirikisho, utabadilishwa pamoja nakuendelezwa hadi Machi 2021.


Viongozi wa nchi za Umoja wa Ulaya hatimaye Jumanne asubuhi walifikia makubaliano ya yuro bilioni 750 za kuufufua uchumi wao. Pesa hizi ni za kukabiliana na athari zilizotokana na janga la virusi vya corona.

Chanjo ya virusi vya Corona inayofanyiwa uchunguzi na wanasayansi wa chuo kikuu cha Oxford nchini Uingereza inaonyesha kwamba ina nguvu za kuongeza nguvu ya kinga mwilini, kulingana na majaribio ya utafiti wa hatua za awali.

Serikali ya Ujerumani Jumatatu ilizishauri nchi wanachama wa Jumuiya ya Afrika mashariki, EAC, kuimarisha mikakati ya pamoja ya kukabiliana na athari za kiuchumi zinazotokana na janga la Corona hasa katika sekta ya utalii.


Share