Jimbo la New South Wales limerekodi kesi mpya 78 za COVID-19 ndani ya jamii, na wakati idadi ya jumla ime pungua, kesi 21 zilikuwa bado ambukizi ndani ya jamii. Biashara zisizo mhimu zimefungwa katika maeneo ya Greater Sydney, na kazi zote za ujenzi zime sitishwa wakati mamlaka wa afya wanalenga, kuvunja uambukizi ndani yama nyumba na sehemu zakazi.
Nalo jimbo la Kusini Australia lita ingia katika siku saba za makatazo kuanzia saa kumi na mbili usiku wa Jumanne 20 Julai kwa masaa ya Kusini Australia. Tangazo hilo limejiri wakati mlipuko wa kesi za COVID-19 zimeongezeka hadi tano, baada ya mtu aliye lia ndani ya mgahawa katika sehemu ya uambukizi mjini Adelaide, kupatwa na virusi hivyo.
Mzozo unaohusu idara za mahakama na bunge, unaendelea kutokota baada ya jaji mkuu Martha Koome kuliandikia bunge kudhibiti maafisa wa mahakama. Mzozo unaohusu idara mbili za serikali nchini Kenya, idara ya mahakama na bunge, unaendelea kutokota baada ya jaji mkuu Martha Koome kuliandikia bunge kudhibiti maafisa wa mahakama kufika mbele kamati ya bunge kuhusu uhasibu kuelezea suala la kuwapo maafisa wengi katika nafasi za ukaimu.