Taarifa ya habari 2 Agosti 2020

Bango la Idhaa ya Kiswahili ya SBS

Bango la Idhaa ya Kiswahili ya SBS Source: SBS Swahili

Jimbo la Victoria lime ingia katika hali ya janga na hatua ya nne ya vizuizi vya coronavirus, kwa ajili yakupunguza usafiri ndani ya jimbo hilo pamoja nakuzuia maambukizi ndani ya jamii.


Kiongozi wa jimbo la magharibi Australia, amesema anataka soko la ajira jimboni humo lipone janga la COVID-19 haraka iwezekanavyo. Serikali ya jimbo hilo imetoa mfuko ajira kwa sekta ya michezo yenye thamani ya dola milioni 300, kama sehemu ya uwekezaji mpana.

Serikali ya Kenya imetangaza Jumamosi kuwa imefanya mazungumzo na Tanzania, kusuluhisha mgogoro ulioibuka Ijumaa, baada ya Tanzania kutangaza kusimamisha ndege za shirika la ndege la Kenya, Kenya Airways (KQ) kufanya safari nchini humo.

Umoja wa Falme za Kiarabu umezindua oparesheni katika kiwanda cha kwanza cha nyuklia kwenye nchi hiyo ya Uarabuni pwani ya ghuba mashariki tu mwa Qatar.


Share