Taarifa ya Habari 19 Oktoba 2021

Bango la taarifa ya habari la SBS Kiswahili

Bango la taarifa ya habari la SBS Kiswahili Source: SBS Swahili

Jimbo la NSW lafanya uwekezaji wakihistoria kukabiliana na visa vya unyanyasaji wa nyumbani.


Takriban $500 milioni zita tumiwa kuwasaidia watu wanao kimbia unyanyasaji wa nyumbani jimboni New South Wales, kama sehemu ya uwekezaji mkubwa wakukabiliana na sababu kubwa ya ukosefu wa makazi kwa wanawake na watoto. Kiongozi wa jimbo hilo Dominic Perrottet amesema, serikali itatoa $484.3 milioni kukabiliana na swala hilo. Hela hizo zitatolewa kwa huduma za misaada, makazi 75 yawanake na nyumba 200 zakodi nafuu kwa wanawake wanao pitia uzoefu wa unyanyasaji wa nyumbani. Huo ni uwekezaji mkubwa zaidi waku maliza unyanyasaji wakifamiia katika historia ya jimbo hilo.

Victoria imetambua kesi mpya 1749 za maambukizi ya coronavirus pamoja na vifo 11 leo Jumanne, katika wiki ambayo vizuizi vya COVID-19 vinatarajiwa kuregezwa. Tarehe 5 Novemba, wakati jimbo hio linatarajiwa kufikisha kiwango cha 80% ya chanjo mbili, Melbourne na kanda ya Victoria zitakuwa chini ya sheria moja. Kiongozi wa jimbo hilo Daniel Andrews amesema umma wa jimbo hilo, una mahitaji magumu kwa hiyo, ana achia dola milioni 21 kusaidia watu wanao kabiliwa na vizuizi kupata chanjo jimbni Victoria.

Jenerali Colin Powell, mtu Mweusi wa kwanza kushikilia wadhifa wa Waziri wa Mambo ya Nje wa Marekani na aliyekuwa mwenyekiti wa Wakuu wa Vikosi vya pamoja vya jeshi, amefariki Jumatatu kutokana na matatizo ya COVID-19. Alikuwa na umri wa miaka 84. Familia yake imetangaza kifo chake kupitia Ukurusa wa Facebook, wakisema, “Tumempoteza mtu muhimu, mume mpenzi, baba, babu na Mmarekani shupavu.” Familia hiyo imesema kuwa Powell alipata chanjo kamili dhidi ya virusi vya corona na kuwashukuru wafanyakazi wa hospitali katika Kituo cha Matibabu cha Taifa cha Walter Reed nje ya Washington “kwa kumpa huduma nzuri” wakati wa siku zake za mwisho. Powell alikuwa mwanadiplomasia wa ngazi ya juu nchini kutoka mwaka 2001 hadi 2005 wakati wa awamu ya kwanza ya Rais wa Republikan George W. Bush.


Share