Kansela wa Ujerumani Angela Merkel amesema leo kuwa kuna uwezekano wa viongozi wa Umoja wa Ulaya kutoafikia makubaliano katika siku ya tatu ya mazungumzo kuhusu mipango ya kuimarisha chumi za mataifa ya Umoja huo ambazo zimeathirika kutokana na janga la virusi vya corona.
John Robert Lewis, shujaa wa kupigania haki za kiraia kwa ajili ya Wamarekani Weusi na Mwakilishi wa muda mrefu katika Baraza la Wawakilishi Marekani, amefariki akiwa na umri wa miaka 80.
Watu wakongo na waafrika kwa ujumla waomboleza kifo cha msomi, mwanasiasa na mwanaharakati profesa Ernest Wamba dia Wamba, aliyefariki Mbanza Nugu huko Jamhuri ya kidemokrasia ya Kongo.