Taarifa ya Habari 18 Julai 2021

Bango la taarifa ya habari la SBS Kiswahili

Bango la taarifa ya habari la SBS Kiswahili Source: SBS Swahili

Mamlaka jimboni Victoria hawaja tupilia mbali wazo laku ongeza muda wa siku tano za makatazo, baada yakurekodi kesi zingine mpya 17 za coronavirus.


Malipo ya msaada wa mapato ya hadi $600, kwa sasa yanatolewa kwa wafanyakazi wanao stahiki jimboni New South Wales. Shirika la Services New South Wales, lita kubali madai ya hadi $15,000 kutoka biashara zinazo athiriwa na vizuizi.

Waumini wa dini laki Islamu wata hamishia sherehe zao mtandaoni wiki hii, kwa sherehe yaki Islamu ya Eid-al-Adha chini ya vizuizi vya COVID-19 jimboni New South Wales. Takriban wakaaji laki sita katika vitongoji vya Fairfield, Canterbury-Bankstown na maeneo ya vitongoji vya Liverpool, hawaezi ondoka katika maeneo hayo kufanya kazi isipokuwa kama wanafanyakazi katika sekta ya afya au huduma za dharura.

Rais wa Afrika Kusini, Cyril Ramaphosa, Ijumaa amedai uporaji na vurugu mbaya ambazo zimetikisa nchi hiyo kwa kipindi cha wiki moja sasa zilipangwa. Amesema hayo alipowasili katika kitovu cha machafuko hayo ambayo yamepelekea maafa na uharibifu mkubwa wa mali tangu rais wa zamani wa nchi hiyo, Jacob Zuma, kujisalimisha kwa polisi na kuanza kifungo cha miezi kumi na mitano, gerezani. Maduka na maghala ya kuhifadhia bidhaa yameporwa katika majimbo mawili na kusababisha hofu ya upungufu wa bidhaa jambo ambalo ni pigo kubwa kwa uchumi wa nchi hiyo. Watu wasiopungua 117 wamefariki, baadhi wakipigwa risasi na wengine kuuawa katika mkanyagano, wakati wa uporaji.


Share