Taarifa ya habari 18 Agosti 2020

Bango la taarifa ya habari la SBS Kiswahili

Bango la taarifa ya habari la SBS Kiswahili Source: SBS Swahili

Wanawake wawili walionyimwa ruhusa yakuingia katika jimbo la Magharibi Australia, warushwa korokoroni kwaku kimbia hoteli yao ya karantini.


Kansela wa Ujerumani Angela Merkel leo ameelezea wasiwasi wake juu ya kuongezeka kwa maambukizi ya virusi vya corona nchini Ujerumani lakini amesema mwenendo wa hali hiyo unaweza kudhibitiwa.

Wizara ya Fedha ya Marekani inayodhibiti Mali za Marekani Nje ya Nchi (OFAC) imewawekea vikwazo raia wanne wa Uganda kufuatia amri ya kiutendaji nambari 13818 inayoimarisha na kutekeleza Sheria ya Kimataifa ya Uwajibikaji wa Haki za Binadamu ya Magnitsky.

Maaskofu wa Kanisa Katoliki na chama cha wanasheria nchini Zimbabwe wameikosoa serikali kwa tuhuma za ukiukwaji wa haki za binadamu na ukamataji wa wapinzani, huku wasi wasi ukiongezeka juu ya namna serikali inavyowatendea wapinzani na mzozo mbaya wa kiuchumi.


Share