Jimbo la Victoria linachunguza uwezekano wakuwasilisha mfumo mpya wa karantini kama mbadala, kwa mfumo wa karantini hotelini katikati ya mji wa Melbourne. Kiongozi wa jimbo hilo Daniel Andrews amesema kundi lamaafisa wa ngazi ya juu, linachunguza vituo viwili ambavyo vike nje ya mji.
Mwanasiasa maarufu nchini Tanzania na visiwani Zanzibar Dk.Mohammed Seif Khatib amefariki dunia leo Jumatatu asubuhi mjini Unguja. Taarifa za kifo chake zimethibitishwa na Mkurugenzi wa maelezo visiwani Zanzibar Dk Juma Mohammed.
Shirika la Afya Duniani, WHO, limeeleza wasiwasi wake kutokana na kuibuka tena kwa ugonjwa wa Ebola huko Afrika Magharibi na kuanzisha mara moja juhudi za kukabiliana na mlipuko huo. Wizara ya Afya ya Guinea ilitangaza mlipuko huo Jumapili miaka mitano baada ya taifa hilo kutangaza kwamba hakuna tena Ebola nchini humo.