Taarifa ya habari 16 Agosti 2020

Bango la taarifa ya habari la SBS Kiswahili

Bango la taarifa ya habari la SBS Kiswahili Source: SBS Swahili

Jimbo la kusini Australia litakuwa sehemu la jaribio lakuanzisha tena safari zakimataifa, jimbo hilo linapo anza kusafirisha mazao ng'ambo pamoja nakuwakaribisha wanafunzi wakimataifa.


Marekani imeshindwa Ijumaa kupata ridhaa ya kuongeza muda wa vikwazo vya silaha dhidi ya Iran vinavyofikia ukingoni, kukiwa na uwezekano wa Washington kulazimisha vikwazo vya zamani vya kimataifa dhidi ya Iran kurejeshwa mara moja.

Watoto watatu wameuawa na watu wengine wanane wajeruhiwa katika shambulizi la guruneti, lililotokea Alhamisi asubuhi katika mtaa mmoja nje ya mji mkuu Bujumbura, Burundi gazeti la mtandaoni la SOS media limeripoti.

Mvua kubwa na mafuriko imeuwa watu 65 na kuharibu makaazi ya zaidi ya watu 14,000 nchini Sudan.


Share