Zaidi ya kesi mpya 400 za COVID-19 ndani ya jamii, pamoja na vifo vinne vya ziada vimerekodiwa jimboni humo.
Makatazo ya jimbo nzima, ambayo yame anza leo jumapili 15 Agosti, yanafunika eneo zima la kanda ya New South Wales. Darriea Turley ndiye meya wa Broken Hill, amesema eneo hilo lilistahili kuwa chini ya makatazo hayo wiki kadhaa zilizo pita.
Wanamgambo wa Taliban wamekaribia kuithibiti nchi nzima ya Afghanistan, huku mji mkuu wa nchi hiyo Kabul ukiwa umedhibitiwa pia na serikali.Mapema leo Jumapili wanamgambo hao wameinyakua Jalalabad, bila mapigano. Jiji hilo lipo Mashariki mwa nchi. Hatua hiyo ilifuatia kudhibitiwa kwa kwa miji muhimu wa shughuli za kiseriali wa Mazar-i-Sharif uliopo kaskazini hapo jana Jumamosi.