Taarifa ya habari 14 Julai 2020

Bango la taarifa ya habari la SBS

Bango la taarifa ya habari la SBS Source: SBS

Afisa mkuu wa afya wa Victoria aonya kuwa hivi karibuni kutakuwa visa hatari zaidi vya watu wenye COVID-19, jimboni humo ambao watahitaji kulazwa hospitalini.


Shirika la Afya Duniani sasa linaonya kuwa janga la COVID-19 linaendelea kuwa baya zaidi ulimwenguni na kwamba huenda hali ya kawaida iliyokuwepo zamani isirejee hivi karibuni.

Vikosi vya usalama nchini Uganda vinafanya msako kwa waandishi wa habari ambao wanafuatilia na kutoa changamoto dhidi ya utawala wa miaka 34 wa Rais Yoweri Museveni.

Rais Ibrahim Boubacar Keita wa Mali anakabiliwa na shinikizo la kuchukua uamuzi muhimu baada ya upinzani kukataa mapendekezo yake mapya.


Share