Taarifa ya Habari 13 Julai 2021

Bango la taarifa ya habari la SBS Kiswahili

Bango la taarifa ya habari la SBS Kiswahili Source: SBS Swahili

Serikali za shirikisho na jimbo la New South Wales, zimetangaza mfuko wa pamoja wa msaada wakiuchumi, kwa watu binafsi na biashara ambazo zime athiriwa na makatazo ya maeneo ya Greater Sydney.


Malipo kwa jina la COVID-19 Disaster Payment, yataongezeka kutoka wiki ya nne ya makatazo hadi $600 kama mtu alipoteza massa 20 au zaidi ya kazi kwa wiki au, $375 kama mtu amepoteza kati ya masaa nane au chini ya 20 ya kazi.

Dazeni yawakaaji wa Kusini Australia wanalazimishwa kujitenga, baada ya wafanyakazi walio kuwa na virusi kutoka NSW kutembelea kituo cha petroli katika kanda hiyo. Idara ya Afya ya Kusini Australia imetambua kituo cha pretroli cha Shell katika eneo la Tailem Bend, ambacho kiko kilomita 97 kusini mashariki ya mji wa Adelaide kama eneo la maambukizi. Watu wanao ingia jimboni humo kutoka maeneo ya kanda, lazima wafanyiwe vipimo vya COVID-19 katika siku ya kwanza yakuwasili, siku ya 5 na siku ya 13 ila haitakuwa lazima kwao kuingia katika karantini. Wakaaji ambao wanajitenga kwa sasa baada yakurejea kutoka kusini mashariki Qld, wataweza ondoka nyumbani kwao Ijumaa.

Mahakama moja ya Afrika Kusini Jumatatu ilianza kusikiliza rufaa iliyowasilishwa na Rais wa zamani wa nchi hiyo Jacob Zuma. Mahakama moja ya Afrika Kusini Jumatatu ilianza kusikiliza rufaa iliyowasilishwa na Rais wa zamani wa nchi hiyo Jacob Zuma juu ya kifungo chake kirefu gerezani kufuatia maandamano makali dhidi ya kufungwa kwake.

 

 

 


Share