Taarifa ya Habari 12 Oktoba 2021

Bango la taarifa ya habari la SBS Kiswahili

Bango la taarifa ya habari la SBS Kiswahili Source: SBS Swahili

Kiongozi wa New South Wales Dominic Perrottet amesema uponaji wa biashara, utakuwa lengo kuu la serikali katika miezi ijayo. Jimbo hilo lilirekodi kesi mpya 360 za COVID-19 pamoja na vifo vitano hii leo Jumanne 12 Oktoba.


Wakaaji wa ACT wata ondoka katika amri zakubaki ndani Alhamisi wiki hii kuanzia saa tano dakika hamsini na tisa za usiku, hiyo ni baada ya wilaya hiyo kufikisha 72% ya chanjo kamili. Mikusanyiko ya nje itaweza hudhuriwa na watu 25, watu watano wanaweza tembeleana nyumbani na idadi ya wateja 50 wanaweza tumia sehemu za nje katika migahawa.Kiongozi wa wilaya hiyo Andrew Barr anawakumbusha watu ambao wako katika wilaya hiyo, idadi ya kesi zinatarajiwa kuongezeka wakati vizuizi vinaregezwa ila, chanjo zinatoa kinga fanisi.

Victoria imerekodi kesi mpya 1466 za maambukizi ya COVID-19 pamoja na vifo nane, hiyo ikiwa ni siku ya pili mfululizo ambayo idadi ya kesi jimboni humo ime shuka. Idara ya afya ya jimbo hilo imethibitisha kuwa kuna kesi 19,627 zinazo shughulikiwa jimboni humo, baada ya idadi ya vipimo 68,509 kufanywa. Kiongozi wa jimbo hilo Daniel Andrews, ame waomba watu ambao wanaweza fanya chanjo zao za pili mapema, wafanye hivyo haraka iwezekanavyo.

Umoja wa Afrika unasema utaongeza na kupanua operesheni zake za kijeshi za kupambana na makundi ya Kiislam yenye mahusiano na Al-Qaeda nchini Somalia na kujumuisha nchi zingine wanachama, wakati muda wake wa hivi sasa unakaribia kumalizika ifikapo Desemba 31. Taifa hilo la Pembe ya Afrika limekabiliwa na ukosefu wa utulivu tena katika miezi ya hivi karibuni, na ucheleweshaji wa uchaguzi uliodumu kwa muda mrefu na mvutano unaoendelea kati ya rais wake na waziri mkuu ikiondoa lengo lake kutoka kwenye kupambana na uasi unaofanywa na wapiganaji wa Al-Shabaab.


Share