Wanasiasa wengi na watalamu wa Marekani wamekosoa uamuzi wa Rais Donald Trump kuiondoa Marekani kutoka Shirika la Afya Duniani (WHO).
Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) ambaye pia ni mgombea urais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. John Pombe Magufuli amewaasa wananchi wa Zanzibar kumchagua Dkt. Hussein Ali Hassan Mwinyi kuwa Rais wa Serikali ya Mapinduzi Zanzibar badala ya kuchagua mgombea wa chama cha upinzani ambaye bila kumtaja jina, rais Magufuli amesema ni mzee na amekuwa akigombea kila mara na anashindwa.
Rais wa Mali anayekabiliwa na misukosuko Ibrahim Boubacar Keita, ametangaza kuvunjiliwa mbali mahakama ya katiba katika juhudi za kuzima machafuko yanalolikumba taifa hilo huku viongozi zaidi wa upinzani wakikamatwa.