Taarifa ya habari 12 Januari 2021

Bango la taarifa ya habari la SBS Kiswahili

Bango la taarifa ya habari la SBS Kiswahili Source: SBS Swahili

Kaimu waziri mkuu wa Australia Michael McCormack ametupilia mbali ukosoaji kutoka makundi ya watetezi wa haki zabinadam namakundi ya jamii, kwaku rudia madai kuhusu vuguvugu la wanao tetea usawa wa rangi ambao wame elezewa kuwa yana "khera sana".


Shirika la upelelezi la Marekani FBI, limeonya kuhusu uwezekano wa maandaamnao yenye silaha kufanywa kote nchini siku chache kabla ya Joe Biden kuapishwa kuwa rais. Kuna ripoti ya makundi yaliojihami yanapanga kukusanyika katika mabunge ya majimbo yote 50 na Washington DC kuelekea siku ya kuapishwa kwake Januari 20. Hofu hiyo inajiri wakati mipango ya usalama imeimarishwa kwa ajili ya hafla hiyo.

Waganda wanajiandaa kupiga kura siku ya Alhamisi, katika uchaguzi ambamo rais mkongwe Yoweri Museveni anapambana dhidi ya wagombea wengine 10, akiwemo mpinzani wake mkuu, Bobi Wine ambaye nguvu yake ya muziki imekichacharisha chama tawala cha NRM. Waandamanaji kadhaa wa upinzani wameuawa wakati wa kampeni zilizogubikwa na ukandamizaji dhidi ya washirika wa Bobi Wine, ambao mamlaka zinasema wanakiuka masharti ya kudhibiti kuenea kwa ugonjwa wa Covid-19.

Jeshi la Ethiopia limesema Jumapili kuwa limeuwa wanachama 15 kutoka chama cha Tigray People’s Liberation Front, TPLF, huku wengine wanane wakikamatwa. Kwa mujibu wa shirika la habari la Reuters, brigedia jenerali kutoka jeshi la serikali amekiambia chombo cha habari cha serikali kwamba miongoni mwa watu waliokamatwa ni aliekuwa kiongozi wa Tigray, Abay Weldu huku miongoni mwa waliouwawa wakiwa ni pamoja na aliekuwa naibu mkuu wa polisi wa eneo.


Share