Taarifa ya habari 11 Mei 2021

Bango la taarifa ya habari la SBS Kiswahili

Bango la taarifa ya habari la SBS Kiswahili Source: SBS Swahili

Uwekezaji kwa wanawake, huduma yamalezi yawatoto, huduma ya uzeeni, ulemavu na afya ya akili watarajiwa kuwa sehemu kubwa ya bajeti ya taifa


Mamlaka wa afya wa Kusini Australia wanachunguza kama, mwanaume kutoka Victoria aliyepatwa na virusi vya COVID-19 baada yakumaliza muda wa karantini ndani ya hoteli mjini Adelaide, kama alipata virusi hivyo hapo.

Mwanaume huyo alirejea nyumbani kwake katika kitongoji cha Wollert ambacho kiko kaskazini mwa Melbourne tarehe 4 Mei, nakuanza kupata dalili za ugonjwa huo siku nne baadae, kabla yakupatwa na virusi hivyo jana jumatatu tarehe 10 Mei.

Mawakili wanaomwakilisha mshukiwa wa ufadhili wa mauaji ya kimbari ya mwaka 1994 nchini Rwanda, wameomba mashtaka dhidi yake yaondolewe, kwa madai kuwa hayuko katika hali nzuri kiafya kuweza kuendelea na kesi hiyo. Félicien Kabuga, mwenye umri wa miaka 84, alikamatwa mwaka mmoja uliopita nchini Ufaransa, na anazuiliwa mjini The Hague, Uholanzi, akisubiri kesi kuendeshwa katika mahakama, iliyo nchini Tanzania, inayoungwa mkono na Umoja wa Mataifa.


Share