Taarifa ya Habari 11 Julai 2021

Bango la taarifa ya habari la SBS Kiswahili

Bango la taarifa ya habari la SBS Kiswahili Source: SBS Swahili

Kampeni mpya ya matangazo inayowahamasisha wa Australia wachukue chanjo za COVID-19, imezinduliwa na serikali ya shirikisho.


Kampeni hiyo yenye thamani ya milioni kadhaa za dola, inawahamasisha wa Australia wajihami kwa chanjo, wakati chanjo nyingi za Pfizer zimeanza kupatikana. Ujio wa dozi za Pfizer unatarajiwa kuongezeka kwa dozi milioni moja kila wiki kuanzia 19 Julai, na kutakuwa dozi milioni 4.5 hadi Agosti.

Kiongozi wa jimbo la New South Wales Gladys Berejiklian, ametabiri kuwa idadi ya takwimu za maambukizi ya kila siku hivi karibuni itaongezeka mara tatu. Jimbo hilo lilirekodi kifo chake cha kwanza cha COVID-19, mwaka huu pamoja na kesi 77 leo jumapili 11 Julai 2021.

Jimbo la Victoria lita funga mipaka yake na jimbo la New South Wales pamoja na wilaya ya Australian Capital Territory [[ACT]], kuanzia usiku wa manane wa leo jumapili 11 Julai 21, baada ya ongezeko ya kesi za coronavirus. Maeneo yote ya New South Wales na Australian Capital Territory, yatakuwa katika eneo jekundu chini ya mfumo wa ruhusa ya usafiri wa jimbo la Victoria. Wakaaji wa Victoria wenye hati ya eneo nyekundu wanaweza rejea jimboni humo ila, lazima wajitenge maramoja, wapimwe na waingie katika karantini kwa siku 14.


Share