Taarifa ya habari 11 Agosti 2020

Bango la taarifa ya habari la SBS Kiswahili

Bango la taarifa ya habari la SBS Kiswahili Source: SBS Swahili

COVID-19 yadai maisha yawavictoria 19 na vita vya maneno vyalipuka kati ya waziri wa huduma ya uzeeni na sekta husika.


Waziri mkuu wa Lebanon Hassan Diab, Jumatatu usiku alitangaza kujiuzulu kwa serikali yake, kufuatia shinikizo kutoka kwa raia wa nchi hiyo, ambao wamekuwa wakishiriki maandamano kwa siku kadhaa kufuatia milipuko mikubwa mjini Beirut Jumanne wiki jana, iliyosabisha maafa na hasara kubwa.

Raia 19 wameuawa na wawili kujeruhiwa katika mashambulizi yaliyofanywa na wanamgambo kwenye vijiji vitatu vilivyoko jimboni Ituri mashariki mwa Jamhuri ya kidemokrasia ya Congo.

Vyombo vya habari nchini Tanzania Radio na Televisheni vimepigwa marufuku kuanzia sasa kurusha matangazo ya vyombo vya kimataifa hadi pale vitakapo pata kibali maalumu kutoka serikalini.


Share