Wabunge wa Democrats wanapanga kuwasilisha hoja ya kutokuwa na imani na Donald Trump kwa mchango wake katika vurugu za uvamizi wa bunge zilizotokea Jumatano katika bunge la Marekani. Msemaji wa Bunge la Wawakilishi Nancy Pelosi amesema atawasilisha hoja ya kutokuwa na imani na Bwana Trump ikiwa hatajiuzulu mara moja.
Waziri wa Usafiri wa Indonesia anasema Shirika la Ndege la Sriwijaya limepoteza mawasiliano na moja ya ndege zake za abiria mara baada ya kuruka kutoka Jakarta Jumamosi. Ndege SJ182 ilikuwa inaelekea Pontianak katika kisiwa cha Borneo. Zaidi ya watu 50 walikuwa wakisafiri katika ndege hiyo, maafisa wamesema.
Wakuu wa usalama nchini Uganda wameonya wapiga kura nchini humo kutosalia katika kituo cha kupiga kura baada ya kupiga kura yao. Uganda inafanya uchaguzi mkuu alhamisi wiki ijayo. Kampeni za uchaguzi zimeshudia machafuko, vifo na kukamatwa kwa wafuasi na wagombea wa upinzani.