Mweka hazina wa taifa Josh Frydenberg amesema nyakati ngumu kwa uchumi wa Australia, zina athirishughuli ila, ana amini kuwa uchumi utapona. Ameongezea kuwa kujiamini kwa watumiaji na matumizi kwa sasa yako juu kwa sasa kuliko mapema mwaka jana, wakati janga lili anza. Ametoa kauli hiyo wakati kuna mjadala unao endelea kuhusu kurejesha malipo ya JobKeeper, serikali ikishtumiwa yakuwa na vigezo viwili wakati zaidi ya idadi yawatu elfu 11, walipokea barua kutoka Centrelink zikidai kuwa walikuwa wame lipwa hela zaidi kwa kupokea malipo ya JobKeeper. Wakati huo huo, baadhi ya biashara zilizo pokea malipo ya JobKeeper ila zilipata faida, hazita hitajika kurejesha hela ambazo zilipokea.
Utawala wa Bidhaa za Matibabu ya Australia imetoa idhini ya muda kwa matumizi ya chanjo ya COVID-19 ya Moderna. Serikali imepata dozi milioni 25 na inatarajia chanjo milioni 10 za Moderna, kuwasili nchini kabla ya mwisho wa mwaka huu wa 2021. Waziri wa Afya Greg Hunt amezungumza na makala ya The Today Show ya runinga ya Channel Nine, na amesema kuwa chanjo ya Moderna imepewa ruhusa ya muda kuwa ni salama kwa matumizi kwa wa Australia wenye miaka 18 na zaidi.
Nchini wanachama wa IGAD wamefanya mkutano wa dharura kuhusu hali iliyopo Sudan Kusini. Hatua hii inafuatia mapigano yaliyozuka mwishoni mwa wiki baina ya makundi ya mrengo wa jeshi wa chama cha Makamu Rais wa kwanza Riek Machar, ikiripotiwa kuwepo na watu waliopata majeraha makubwa. Mawaziri wa mambo ya kigeni wa nchi wanachama wa mamlaka ya kieneo ya serikali na maendeleo (IGAD) wamefanya mkutano wa dharura hii leo, kufuatia mgawanyiko mkubwa uliotokea, ndani ya chama cha SPLA-IO cha Sudan Kusini, huku Washirika wa Riek Machar wakiendelea kulaani majenerali waliotangaza kuondolewa kwake madarakani.