Waziri katika baraza la mawaziri la Uingereza Michael Gove amesema muda wa mwezi mmoja wa kufunga kabisa shughuli za kichumi za taifa hilo katika kukabiliana na virusi vya corona unaweza kuongezwa.
Rais mteule wa Tanzania John Pombe Magufuli hatimaye amepokea cheti cha ushindi wake katika uchaguzi wa urais uliokamilika. Wakati huo huo vyama vikuu viwili vya upinzani nchini Tanzania, vimetaka kurejewa kwa uchaguzi mkuu wa nchi hiyo, na vilevile kutoa wito kwa Watanzania kufanya maandamano yasiyo na kikomo, kuanzia Jumatatu hadi matakwa yao yatakapotekelezwa.
Rais wa zamani wa Ivory Coast Laurent Gbagbo ameonya kwamba taifa hilo la Afrika magharibi linaweza kuingia kwenye machafuko makubwa iwapo wagombea kwenye uchaguzi wa jumamosi, hawatosuluhisha mvutano uliosababisha maandamano ya vurugu na wito wa upinzani wa kususia uchaguzi.