Wengi wao wamepoteza ajira zao kwa sababu ya janga hilo, na wengine wamekwama nchini Australia baada ya mipaka kufungwa kudhibiti usambaaji wa maambukizi hayo katika jamii.
Viongozi wa shirika la GLAPD walipokea maombi mengi ya msaada kutoka kwa jamii, hali ambayo ilisababisha wazindue mradi wakutoa vyakula na misaada mingine kwa watu ambao wamepoteza kazi na wanakabiliwa na changamoto zakumudu maisha yakila siku, katika mradi wakujaza mifuko ukarimu.