Wakati wengi wao hupokea msaada kutoka serikali au familia zao, wanafunzi wengi wakimataifa humudu gharama za maisha, kupitia kazi katika makampuni namashirika mbalimbali.
Wanafunzi wakimataifa ni miongoni mwa makundi katika jamii, yaliyo hisi madhara makubwa zaidi ya janga la COVID-19. Je vizuizi pamoja na hatua zingine, ambazo zimechukuliwa na serikali zamajimbo nchini kukabili janga hili, zimewaacha wanafunzi wakimataifa katika hali gani?
Sharon ni mmoja wa wanafunzi wakimataifa mjini Melbourne, alichangia uzoefu wake wa vizuizi na hatua ambazo serikali ya jimbo la Victoria, imechukua kukabili janga hili. Bofya hapo juu kwa taarifa kamili.