Makosa hayo nisehemu ya mjadala mpana kuhusu mbinu gani, itakuwa bora kutoa taarifa kwa jamii zenye tamaduni na lugha tofauti kuhusu hatari za COVID-19.
Waandishi wa utafiti wa Chuo cha Monash wanapendekeza tume yaushauri yakitaifa iundwe, kwa ajili yakusaidia mamlaka kuunda ujumbe waki afya wa umma, kwa matumaini yakuongeza nguvu ushirikiano wa sasa.
Mapema mwaka huu, serikali ya shirikisho ilitupilia mbali taarifa kuwa, ilifeli kushauriana ipaswavyo na jamii zawahamiaji, wakati ilikuwa iki toa jibu kwa janga hili.
Tarehe 27 Agosti viongozi wajamii mbali mbali, wanatarajiwa kutoa ushahidi katika uchunguzi wa kikao cha bunge la Victoria, kwa jinsi serikali ya jimbo hilo ilivyo jibu janga la coronavirus.
Na unaweza endelea kupata taarifa mpya kuhusu coronavirus katika lugha yako kwenye tovuti hii: sbs.com.au/coronavirus.