Serikali ya shirikisho yakana inampango wakutoa nyongeza yakudumu yamalipo ya JobSeeker

Protests over JobKeeper

Source: AAP

Serikali ya shirikisho inakana ripoti kuwa inazingatia ongekezo lakudumu kwa malipo ya JobSeeker.


Sasa serikali inakabiliana na wito wakutekeleza uvumi huo wa jeki kwa malipo hayo ya ustawi.

Mweka hazina wa shirikisho Josh Frydenberg anatarajiwa kutangaza bajeti ndogo tarehe 23 ya Julai, ambapo ataweka wazi maelezo kuhusu mfumo wa JobSeeker.

Tangazo hilo litajumuisha pia hatma ya mfumo wa JobKeeper kupitia Septemba, baada ya tathmini ya mfumo wa ruzuku ya mapato, iliwasilishwa hivi karibuni kwa serikali.

Na unaweza endelea kupata taarifa mpya kuhusu coronavirus katika lugha yako kwenye tovuti hii sbs.com.au/coronavirus.


Share