Sen Mutula Kilonzo Jr: "Hauwezi jenga daraja wakati wengine wanachimba kulibomoa"

Seneta Mutula Kilonzo Jr, akiwasha bungeni

Seneta Mutula Kilonzo Jr, akiwasha bungeni Source: Parliament of Kenya

Wiki hii baadhi yamaseneta wa Kenya, walijipata chini ya shinikizo kutoka kwa vyombo vya usalama nchini humo.


Maseneta wenza walisimama bega kwa bega nao ndani ya seneti, ambako walimhamasisha spika aahirishe kikao walichokuwa ndani, hadi pale wenzao watakapo achiwa huru kuhudhuria vikao pia.

Seneta Mutula Kilonzo Jr, alikuwa katika mstari wa mbele akiongoza kampeni hiyo, na kwa mara ya kwanza alionesha hasira yake hadharani tofauti na anavyo julikana kuwa mtulivu kila mara.

Katika mazungumzo maalum na Idhaa ya Kiswahili ya SBS, Sen Kilonzo Jr alifunguka kuhusu kilicho mkera, hadi akamweleza spika kuwa yuko tayari kufanya kazi hiyo, iwapo spika hayuko tayari kutekeleza wajibu wake.


Share