Sekta yamalezi yawatoto ya Australia, kutoa huduma bila malipo kwa wazazi wanao fanyakazi

Watoto wacheza ndani ya kituo cha huduma ya watoto

Source: SBS

Huduma ya watoto itatolewa bila malipo kwa wazazi ambao, wanaendelea kufanya kazi wakati wa janga la virusi vya Corona.


Serikali ya shirikisho itasaidia vituo vya huduma ya malezi ya watoto elfu 13 ambavyo viko nchini Australia, kwakulipa nusu ya gharama ya oparesheni za vituo hivyo, kwa sharti kuwa vituo hivyo vitabaki wazi bila gharama yoyote kwa familia.

Na serikali ya shirikisho inawekeza dola milioni 123, ambazo zitatumiwa kuzisaidia jamii zawa Australia wakwanza. Hela hizo zita toelwa kwa kipindi cha miaka mbili, kupiga jeki rasilimali za biashara zawa Australia wa kwanza, zita pokea dola milioni 50 katika miezi ijayo.

Endelea kupokea Taarifa mpya kuhusu coronavirus katika lugha yako kupitia tovuti hii: sbs.com.au/coronavirus


Share