Rahab:"Kama unaishi mwenyewe ni vigumu sana, unasikia umelemewa wakati huu wa makatazo ya COVID-19"

Idadi ya vijana ambao wana matatizo ya ugonjwa wa afya ya akili imeongezeka tangu Melbourne iliporejea katika makatazo.

Idadi ya vijana ambao wana matatizo ya ugonjwa wa afya ya akili imeongezeka tangu Melbourne iliporejea katika makatazo. Source: Pixabay

Janga la COVID-19 lina endelea kusababisha changamoto nyingi kwa jamii na mamlaka wanao jaribu kudhibiti maambukizi ndani ya jamii nchini.


Baadhi ya hatua ambazo mamlaka wame chukua kudhibiti maambukizi ya COVID-19 ndani ya jamii, nikuweka amri ya makatazo yakusafiri zaidi ya kilomita 10 kutoka sehemu unako ishi, pamoja na makatazo ya watu kubaki nyumbani isipokuwa kwa sababu kadhaa muhimu, kama kutoa au kopokea huduma mhimu, kuemea, kupokea matibabu au kufanya mazoezi.

Bi Rahab ni mkaaji wa kanda ya Central Coast jimboni New South Wales, yeye pia ni balozi wa shirika linalo simamia maswala ya afya ya akili ndani ya jamii. Katika mazungumzo maalum na Idhaa ya Kiswahili ya SBS, alifunguka kuhusu masaibu ya watu wanao kabiliana na ugonjwa wa akili, wakati huu wa makatazo ya COVID-19.

Bofya hapo juu kwa taarifa kamili.


Share