Waziri Mkuu Turnbull asema atatekeleza mkataba wa Tennant Creek

Waziri Mkuu Malcolm Turnbull akutana na kundi la densi la jamii ya watu wa kwanza wa Australia  baada yakuwasili katika uwanjwa wa ndege wa Tennant Creek katika wilaya ya kaskazini

Waziri Mkuu Malcolm Turnbull, akutana na kundi la densi la jamii ya watu wa kwanza wa Australia katika uwanjwa wa ndege wa Tennant Creek, Wilaya ya Kaskazini. Source: AAP

Waziri Mkuu Malcolm Turnbull amesema atatekeleza mkataba wa serikali na mji wa Tennant Creek ambao uko Katika jimbo la Kaskazini ya Australia.


Mkataba huo unajumuisha ushirikiano mkubwa zaidi kati ya tawi zote za serikali.

Tennant Creek na maswala yake, yame chambuliwa kwa miezi mingi baada ya msichana mwenye umri wa miaka miwili kubakwa mwezi Februari. Waziri Mkuu ameongezea kuwa, swala moja ambalo ni kubwa zaidi ni uhaba wa makazi.

Serikali ya wilaya ya kaskazini imesema inajaribu kukabilian ana uhaba wa kamazi, kwakujenga nyumba tatu kufikia sasa mwaka huu, na kuna nyumba zingine tisa ambazo zinatarajiwa kujengwa kufikia mwisho wa mwaka huu.

Naye waziri wa shirikisho wa huduma za jamii Dan Tehan amesema kwamba, ata zingatia wazo lakuwasilisha jaribio la matumizi ya kadi ya ustahi badala yakuwapa watu hela taslim. Kadi hiyo inafanya kazi kama kadi yakawaida ya benki, na wanao pokea mapato ya ustawi itakuwa lazima waitumie.

Kadi hiyo hubana 80% ya malipo ya wanao pokea malipo ya ustawi, na hela hizo zinaweza tumiwa tu kununua vyakula na vifaa vingine muhimu. Mwenye hiyo kadi hawezi nunua pombe au kucheza kamari.


Share