Taarifa hiyo ime jiri baada yakuzinduliwa kwa kampeni, kuhusu utoaji wa chanjo ya COVID-19.
Wakati huo huo, usafiri bila mahitaji ya karantini kutoko New Zealand kuja nchini Australia, utasitishwa hadi alhamisi ijayo, hatua ambayo imekosolewa na waziri mkuu wa NZ Jacinda Ardern. Bi Ardern ame mweleza waziri mkuu wa Australia Scott Morrison kwamba, amesikitishwa na uamuzi huo, akiongezea kwamba ana amini hali nchini New Zealand imedhibitiwa na anazingatia kufanya mpango wa usafiri na majimbo ya Tasman, badala yakuwa na maafikiano yakitaifa.
Hatua yakusitisha usafiri huo kwa muda, umejiri baada ya mwanamke nchihi New Zealand kupatwa na kirusi ambukizi kutoka Afrika Kusini. Kwa hatua za afya na misaada ambayo ipo kwa sasa, katika jibu la janga la COVID-19 katika lugha yako, tembelea tovuti hii: sbs.com.au/coronavirus.