Ila kabla tuanze, onyo kuhusu makala haya. Tuta jadili vipengele vya ukatili wakijinsia ambavyo vinaweza wahuzunisha baadhi yawa sikilizaji.))
Nchini Australia kesi 85 za unyanyasaji wa kijinsia kwa wastan huripotiwa kila siku. Tafiti zimedokeza zaidi ya kijana mmoja kati ya vijana watatu, wamepitia uzoefu unyanyasaji wa kijinsia ambao hawakutaka katika maisha yao.
Kama wewe ni mwathirika mnusurika wa ubakaji, unaweza kuwa ukizingatia kuripoti uzoefu wako kwa mamlaka hatua ambayo itaona mhusika akikabiliana na mfumo wa haki. Ila mara nyingi uamuzi huu, huja na matatizo mengi yakihisia.
Kama una amua au hau amui kuripoti kwa polisi, kuna aina nyingi ya huduma ya misaada unaweza pata. Kama wewe au mtu unaye jua ame athirika kwa unyanyasaji wa kijinsia, piga simu kwa namba hii 1800RESPECT. Unaweza pigia simu pia Lifeline kwa namba hii: 13 11 14 au Beyond Blue kwa namba hii 1800 22 46 36.