Sehemu moja ya jamii ambayo ime kumbwa zaidi na madhara ya makatazo hayo, ni wajasiriamali ndani ya jamii, ambao wame weka wazi changamoto wanazo kabiliana nazo wakati huu wa makatazo.
Bi Nava ni mjasiriamali katika kitongoji cha Fairfield jimboni New South Wales, yeye ni miongoni mwa maelfu ya wajasiriamali ambao ongozeko ya vurusi vya COVID-19 ndani ya jamii imesababisha biashara zao zifungwe kwa muda, mamlaka waki jaribu kudhibiti usambaaji wa virusi hivyo ndani ya jamii.
Katika mazungumzo maalum na Idhaa ya Kiswahili ya SBS Bi Nava, alifafanua jinsi makatazo hayo yame athiri biashara yake na hasara ambazo amepata. Bonyeza hapo juu kwa taarifa kamili.