Wakati huu wa janga la corona pamoja na vizuizi ambavyo mamlaka wame weka kukabili usambaaji wa virusi hivyo katika jamii, mashirika kama Nakango Vision yana fursa yakipekee kuregeza pigo ambalo jamii nyingi zimepokea kupitia vizuizi vyakukabiliana na COVID-19.
Nava Azu Ozegbe ndiye rais wa shirika la Nakango Vision, katika mazungumzo maalum na Idhaa ya Kiswahili ya SBS, aliweka wazi hatua ambazo shirika lake limechukua kuhakikisha jamii inayo tegemea msaada wa shirika lake inaendelea kuhudumiwa.
Kwa taarifa ya zaida kuhusu shirika la Nakango Vision tazama tovuti yao: www.nakangovisions.org