Mwongozo wa Makazi: Usaidizi wa masomo ya mtoto wako nyumbani

Mzazi achunguza kazi za shule za wanawe

Mzazi achunguza kazi za shule za wanawe Source: Getty Images

Wakati waziri mkuu anataka shule zote zifunguliwe tena mnamo mwezi Juni, wazazi wengi wanawaweka watoto wao nyumbani kwa wasiwasi wa usalama wao.


Kwa bahati nzuri kwa wazazi hao, rasilimali na msaada wa kujifunza nyumbani unapatikana ikiwa utahitajika.

Wanafunzi katika jimbo la New South Wales wataanza kuhudhuria shule siku moja kwa wiki kuanzia Jumatatu Mei 11. Wanafunzi wa mwaka wa 12 watarudi shuleni wakati shule za umma zinaanza kufundisha uso kwa uso kwa wakati mmoja.

Huko Australia Magharibi, shule ziko wazi kwa wazazi na walezi wote ambao huchagua kupeleka watoto wao.

Shule zote za serikali za Victoria zinatoa mpangilio rahisi wa kujifunza mtandaoni wakati wa muhula wa pili. Wanafunzi ambao wanaweza kujifunza kutoka nyumbani wanaombwa kukaa majumbani.

Tasmania imewataka wanafunzi waendelee kusomea nyumbani kadri inapowezekana. Shule za maeneo ya kaskazini, kaskazini-magharibi na kusini zimefunguliwa kwa wanafunzi ambao hawawezi kusimamiwa nyumbani.

Wanafunzi wa Australia Kusini wanahimizwa kuhudhuria shule kwani viwango vya maambukizi viko chini. Wanafunzi wote wa jimbo la Kaskazini wanatarajiwa kuhudhuria mashuleni.

Kwa wanafunzi wa shule ya msingi wa Queensland , Mwaka wa kwanza, Mwaka wa kumi na moja na kumi na mbili, shule zitaanza tena kuanzia Jumatatu Mei 11. Wanafunzi wa mwaka pili hadi wa kumi ambao wana uwezo wa kusimamiwa nyumbani na kujifunza kutoka nyumbani wanapaswa kukaa nyumbani.

Shule za mji mkuu wa Australia zinafundisha mtandaoni wakati wa muhula wa pili. Shule tisa zinatoa usimamizi maalumu kwa watoto wa wafanyakazi muhimu.

Kwa habari zaidi juu ya rasilimali za kujifunza nyumbani, tembelea tovuti zifuatazo.

ACT https://www.education.act.gov.au/public-school-life/remote-learning-in-term-2-2020

https://www.education.act.gov.au/schooling/learning-resource-library

NSW https://education.nsw.gov.au/teaching-and-learning/learning-from-home/wellbeing-at-home/parents-and-carers

Northern Territory https://education.nt.gov.au/publications/information-for-term-2-2020?SQ_VARIATION_814972=0

Queensland https://education.qld.gov.au/curriculum/learning-at-home

South Australia

https://www.education.sa.gov.au/teaching

Tasmania https://www.education.tas.gov.au/learning-at-home/

Victoria: https://education.vic.gov.au/parents/learning/Pages/home-learning.aspx

Western Australia: https://www.education.wa.edu.au/learning-at-home


Share