Ikiwa unateseka na unahitaji kuongea na mtu kuhusu hali yako ya ustawi, piga simu Lifeline namba 13 11 14 au wapigie Beyond Blue kwa namba 1300 22 4646 kwa huduma za masaa 24.
Unaweza pia wapigia ofisi ya kodi ya Waustralia kitengo cha Huduma za dharura kwa namba 1800 806 218 hadi saa nne usiku mida ya Australia Mashariki katikati ya wiki au kuanzia saa nne asubuhi hadi saa nne usiku mwishoni mwa wiki.
Kitengo cha taarifa cha Watetezi wa wafanyabiashara ndogondogo na familia kitakuwa wazi kuanzia saa mbili asubuhi hadi saa mbili usiku, Jumatatu hadi Ijumaa kwa namba 1300 650 460. Kwa msaada wa lugha, piga kitengo cha huduma za kutafsiri na ukarimani kwa namba 13 14 50.