Mwongozo wa Makazi: Kuishi karibu na jamii yangu

Jamii yajumuika kuandaa nakuchangia chakula

Jamii yajumuika kuandaa nakuchangia chakula Source: Getty Images

Baada ya kuhamia katika nchi mpya, kuna mengi ya kupanga na mambo mengi mapya ya kujifunza.


Hata kama umekuwa hapa Australia kwa miaka, labda bado unakutana na hali ambazo hauelewi kabisa.

Haishangazi kwamba wahamiaji wengi wapya wanaamua kuishi karibu na jamii yao ili kufanya mambo yawe rahisi. Lakini je! Kuishi karibu na jamii yako ndio chaguo bora kwako kila wakati?

Wahamiaji wengi wananufaika kutokana na kupata msaada kutoka kwa jamii yao, haswa wanapokuwa wapya kwenye nchi. Lakini kuunda uhusiano na Waaustralia wengine ni muhimu sana.


Share