Mwongozo wa Makazi: Jinsi yakuwasilisha marejesho yako ya ushuru 2020

wakati wa marejesho ya ushuru

wakati wa marejesho ya ushuru Source: SBS

Ikiwa umepata mapato nchini Australia kati ya tarehe 1 mwezi Julai 2019 hadi Juni 30, utahitaji kuingiza maombi ya marejesho ya ushuru ifikapo 31 Oktoba 2020.


Hapa kuna njia kadhaa ambazo unaweza kudai kurejeshwa kwa ushuru na kupunguza mswada wako wa ushuru kwa mwaka wa fedha.

ATO imeshafanya kazi na mashirika ya kijamii karibu 700 ya kitamaduni na lugha tofauti kusambaza taarifa za ushuru. Unaweza kujifunza juu ya taarifa za kodi kwenye mazungumzo ya Ushuru ya ATO tovuti katika lugha yako au pia simu kwa ushauri ATO kutumia namba 13 28 61.

Unaweza pia kustahiki Usaidizi wa Ushuru bure ikiwa unapata pato la chini ya $60,000.

Ikiwa unahitaji msaada wa lugha, piga Huduma ya Utafsiri na Ukarimani kupitia 13 14 50 na omba kuunganishwa na huduma ya msaada kwa njia ya simu ya ATO.

Tembelea tovuti ya ATO kwa taarifa juu ya hatua za ushuru na msaada kwa biashara na watu binafsi wakati huu wa janga la COVID-19.


Share