Mwongozo wa Makazi: Je! Mikopo ya kila siku na janga hili italeta 'tsunami ya madeni'?

Debt Collection

Source: AAP

Kuporomoka kwa uchumi wa kwanza wa Australia katika miaka 29, kumewafanya washauri wa masuala ya fedha kushughulika na kupokea simu kutoka kwa watu ambao, hawajawahi kukabiliwa na matatizo ya madeni.


Kuna wasiwasi pia madeni wakati wa janga hili, yanaweza sababisha wasiwasi mkubwa kwa afya ya akili.

Unaweza kupata mtoa huduma wako aliyechaguliwa kwa msaada wa mkalimani kwa kupiga huduma ya utafsiri na ukarimani kupitia namba 13 14 50. Ikiwa unakabiliwa na msongo wa mawazo na unahitaji msaada, wasiliana na Beyond Blue kupitia 1300 22 4636 au piga simu shirika la Lifeline kwa namba 13 11 14.

Kwa ushauri wa bure na wa siri wa kifedha na kisheria, wasiliana na Nambari ya Msaada wa Madeni ya Kitaifa kupitia namba 1800 007 007. Kwa taarifa zaidi au shirika la Good Shepherd lisilo na riba, wala ada ya mikopo, tembelea tovuti yao au piga simu namba 1300 121 130.


Share