Kura hiyo iligundua kuwa karibu watu wanane kati yawatu kumi wa Australia, walidhani ushoga unapaswa kukubaliwa na jamii.
Walakini, wanaharakati wa kundi la mashoga na masenge lijulikanalo kama LGBTI wanaendelea kutetea haki pana licha ya kuhalalishwa kwa ndoa ya jinsia moja mnamo Desemba 2017.
Ikiwa unahangaika na unahitaji kuongea na mtu sasa hivi, pigia simu kitengo cha msaada cha Lifeline kwa namba 13 11 14, iwapo unakabiliana na mawazo yakujiua unaweza pata msaada ukipigia simu namba hii 1300 659 467, na 1800 737 732. Na namba ya msaada kwa Watoto ni 1800 55 1800 (kwa Watoto wenye umri kati ya miaka 5 hadi 25). Maelezo zaidi yanapatikana kwenye tovuti ya beyondblue.org.au na tovuti ingine ya lifeline.org.au.