Mwongozo wa Makazi: Haki na wajibu wako kufanyia kazi nyumbani

Kufanyia kazi nyumbani

Makampuni yawaruhusu wafanyakazi kufanyia kazi nyumbani, kuzuia usambaaji wa coronavirus. Source: Getty

Waaustralia wengi, pamoja na wafanyakazi takribani asilimia 88 toka mashirika kote ulimwenguni, wamelazimika kuzoea mabadiliko ya ghafla ya kufanya kazi wakiwa nyumbani.


Wataalam wanasema ni kwa maslahi ya mwajiri na mwajiriwa, kutunza mazingira salama ya kazi. Tembelea tovuti ya Fair Work Ombudsman kwa maelezo zaidi juu ya haki na majukumu yako katika kipindi hiki cha janga la virusi vya corona.

Ikiwa unaamini umepata virusi, piga simu kwa daktari wako au wasiliana na watoa taarifa za virusi vya Corona kitaifa kwa simu namba 1800 020 080. Ikiwa una msongo wa mawazo na unahitaji msaada piga simu Lifeline kwa namba 13 11 14 or Beyond Blue namba 1300 22 4636 kwa usaidizi masaa 24. Ikiwa uko chini ya umri wa miaka 25, unaweza pia wapigia simu Kids Helpline kwa namba 1800 55 1800 wakati wowote kwa sababu yoyote.

Unaweza pia piga simu kwa huduma ya kitaifa ya Utafsiri na Ukalimani kwa namba hii 1800 131 450, kwa msaada wa lugha kuwasiliana na mashirika unayo taka wasiliana nayo.


Share