Mji wa Cowra waingia katika amri yakuto toka nje, wakati idadi ya kesi za maambukizi yaendelea kuongezeka Victoria

Shamba canola mjini Cowra New South Wales alfajiri

Shamba canola mjini Cowra New South Wales alfajiri Source: Getty Images

Mji wa kanda wa Cowra jimboni New South Wales, uli ingia katika amri yakufungiwa ndani kuanzia saa kumi na moja jioni ya Jumatatu katika jibu wa ongezeko la idadi ya visa vya COVID-19.


Wakati huo huo jimboni Victoria, kume kuwa ongezeko ya idadi ya maambukizi na kwa sasa jimbo hilo limerekodi kesi mpya 567.

Wilaya ya kaskazini nayo imerekodi kesi moja mpya ya COVID-19, baada ya mwanaume mmoja aliye wasili mjini Darwin kutoka New South Wales na akapatwa na virusi hivyo. Mwanaume huyo alipatwa na virusi hivyo Jumapili na kwa sasa, yuko ndani ya kituo chakitaifa kwa jina la Centre for National Resilience, ambacho kiko katika eneo la Howard Springs, karibu ya mji wa Darwin.

Ufuatiliaji wa watu walio kutana na mwanaume huyo unaendelea, na kufikia sasa idadi ya watu 24 wame tambuliwa. Kwa hatua za msaada na afya ambazo zipo, katika jibu la janga la COVID-19 katika lugha yako, tembelea sbs.com.au/coronavirus


Share