Makundi ya waumini yaomba vizuizi vichache kwa ibada

Coronavirus imesababisha usumbufu mkubwa kwa jamii zawaumini nchini Australia.

Coronavirus imesababisha usumbufu mkubwa kwa jamii zawaumini nchini Australia. Source: Aaron Fernandes/SBS News

Waumini ambao wame zuiwa kujumuika katika sehemu za ibada wakati wa vizuizi jijini Melbourne, wameomba wahudumiwe vizuri zaidi katika hatua ijayo yakuregezwa kwa vizuizi.


Watu hao wame gadhabishwa na hatua yakuwaruhusu watu wengi zaidi, kujumuika migahawani, kuliko sehemu za ibada chini ya mchakato wa jimbo la Victoria, wakurejesha hali ya kawaida jimboni humo. Waumini hao wame wasilisha maombi yao kwa kiongozi wa jimbo la Victoria.

Takriban 60% yawa Victoria, walijitambua kama waumini katika sensa iliyo pita.

Viongozi wakidini wanatumai vizuizi vitakavyo regezwa jumapili 18 Oktoba, vitawaletea afueni.


Share