Maelfu wanao pinga makatazo, wakamatwa Melbourne baada yakupambana na polisi

Waandamanaji wanao pinga makatazo wapambana na polisi mjini Melbourne.

Waandamanaji wanao pinga makatazo wapambana na polisi mjini Melbourne. Source: AAP

Zaidi ya idadi ya watu 230 wali kamatwa na maafisa 10 wa jeshi la polisi kujeruhiwa, katika maandamano ya vurugu dhidi ya makatazo mjini Melbourne.


Maandamano hayo yalijiri wakati makatazo yanaendelea katika sehemu za majimbo ya Victoria na New South Wales, majimbo yote mawili yakiongeza juhudi yaviwango vya chanjo kabla yakuregezwa kwa vizuizi.

Dozi za kwanza za chanjo ya jimbo hilo zina endelea kuwa chache kulinganisha namajirani wao, wakiwa na 40% tu miongoni mwa umma unaostahiki. Utabiri mpya kulingana na kasi ya utoaji wa dozi ya pili, unaonesha kuwa jimbo la New South Wales na wilaya ya A-C-T zinatarajia kufikia viwango vya 70% na 80% ya utoaji wa dozi mbili za chanjo kufikia mwisho wa Oktoba.

Kufikia sasa, tarehe hiyo inaonekana nikama itakuwa mwezi mmoja baadae kwa majimbo ya Magharibi Australia, Queensland, na Victoria. Kwa hatua za afya na msaada, ambazo zipo kwa sasa kwa jibu la janga la COVID-19 katika lugha yako, tembelea sbs.com.au/coronavirus


Share