Maandamano yakupinga maandamano hayo yaliyo laani ‘’ukuaji wa itikadi za mrengo wakulia’’ yali andaliwa pia mjini Melbourne.
Matokeo ya hivi karibuni ya kura ya maoni yanaonesha kuwa uungwaji mkono wa Daniel Andrews umeongezeka, wakati wa janga ila wanao andamana dhidi ya muswada wa janga waliwazidi kwa wingi walio andamana kuunga mkono serikali. Pande zote mbili zime ahidi kurejea mitaani tena katika siku zijazo.
Kwa taarifa na msaada uliopo kwa sasa katika jibu la janga la UVIKO-19 katika lugha yako, tembelea tovuti hii sbs.com.au/coronavirus.