Ligi kuu ya Ujerumani yawapa wapenzi wa soka afueni kutoka janga la COVID-19

Wachezaji wa ligi kuu ya soka ya Ujerumani

Wachezaji wa ligi kuu ya soka ya Ujerumani Source: Getty Images

Ligi zote za michezo duniani ziliahirishwa baada ya mlipuko wa Coronavirus kusambaa duniani kote kwa kasi.


Baada ya miezi kadhaa ya uhaba wa michezo duniani kote, serikali nyingi zimeanza kuregeza vizuizi vyakukabiliana na usambaaji wa janga hilo la Coronavirus.

Nchini Ujerumani, mamlaka wametoa ruhusa kwa ligi kuu ya mchezo wa mpira wa miguu nchini humo kuendelea tena hali ambayo itashuhudiwa Jumamosi 16 Mei nchini Australia na duniani kote kupitia runinga. Licha yakurejea kwa timu husika dimbani, mashabiki ambao ni sehemu muhimu ya mechezo wa soka, hawata ruhusiwa kuingia viwanjani timu zao zikicheza kwa sababu za usalama wakiafya.

Mtayarishaji wa michezo wa Idhaa ya Kiswahili ya SBS alichunguza hatua ambazo viongozi husika wamechukua kurejesha wachezaji uwanjani kwa hali salama, hali ambayo itachangia katika harakati zakurejesha hali ya kawaida ya maisha baada ya janga la Corona kusababisha uharibifu mkubwa duniani kote.

 


Share