Kutunza Walezi: Jinsi yakupata huduma za usaidizi wa walezi nchini Australia

aged carer, nursing support worker, skilled occupation list

Credit: envato elements

Takriban mtu mmoja kati yawatu tisa nchini Australia ni walezi, watu ambao huwa hudumia jamaa wao ambao ni wazee, wadhaifu, marafiki, au mtu anaye ishi na hali fulani ya afya au ulemavu.


Ila mara nyingi, walezi wengi hawajitambui hivyo au, wanajua kuna aina ya huduma za misaada zinazo tolewa bure kwao.

Kuna takriban walezi milioni 2.7 nchini Australia. Walezi huja kwa miaka yote, jinsia na aina tofauti za maisha.

Ila, kitu kimoja ambacho walezi wote wanachangia ni kujitolea kwao kuhudimia mtu anaye hitaji msaada ambaye yuko maishani mwao.

Wale ambao wanawahudumia jamaa wao amboa ni wazee, nao pia wanaweza pata taarifa nyingi kupitia jarida la Australian Carer’s Guide, ambalo huchapishwa kila miezi mitatu kwa faida ya walezi.

Bonyeza hapo juu kwa taarifa kamili.

Share