Serikali ya shirikisho ime itisha kura ya maoni kwa wa Australia kuamua, kama wangependa kufanyia katiba mageuzi nakujumuisha 'sauti yawa Australia wa kwanza bungeni'.
Kwa hiyo, kura ya maoni ni nini, nani anastahiki kupiga kura nchini Australia na, Sauit kwa bunge itafanya nini?
Serikali ya shirikisho inawaomba wapiga kura wanao stahiki, wa amue kama wata boresha katiba ya Australia ili iwatambue wa Australia wa kwanza, kupitia tume ya uwakilishi itakayo julikana kwa kimombo kama ‘Voice to Parliament’.
‘The Voice’ litakuwa ni kundi litakalo pigiwa kura kuishauri serikali kuhusu maswala na sheria zinazo wa athiri wa Australia wa kwanza.